August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu: Serikali hii ni ya hovyo

Spread the love

TUNDU Lissu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ameseme kuwa, vitendo vinavyofanywa na serikali ya sasa ni vya hovyo, anaandika Faki Sosi.

Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki amesema hayo leo muda mfupi baada ya kumaliza kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kwenye shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa wengine watatu wanadaiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia gazeti la Mawio la tarehe 14 Januari 2016.

Kwenye gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ Lissu alinukuliwa kama mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa na serikali.

Nje ya mahakamani hiyo Lissu amesema “nchi yetu imeingia katika giza nene, huyu dikteta uchwara, naomba nirudie tena, huyu dikteta uchwara anahitaji kupingwa na kila mwananchi.

“Kila msema kweli wa nchi hii. Huu ni wakati wa kujitokeza na kusema hii ni nchi ya vyama vingi, hii ni nchi inayotambua haki za binadamu kwenye Katiba yake.

“Hatuwezi tukakubali nchi iongozwe kwa kauli za mdomo za mtu mmoja hata kama amechaguliwa kuwa rais,”

Akizungumzia kesi iliyofunguliwa na kuhusishwa kwake Lissu amesema, kesi iliyofunguliwa na serikali dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio ya uchochezi, ni ushahidi tosha kuwa nchi imeingia kwenye giza nene la udekikteta.

Amesema, hata sheria ya magazeti ya mwaka 1976  ipo wazi  kwamba, kuikosoa serikali sio uchochezi.

“Mashtaka haya yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezo, sio ya uchichozi hata kidogo. Nilichosema, niliulizwa na waandishi … niliosema uchaguzi wa marudio ya uchaguzi Zanzibar yanaweza  kuviingiza visiwani hivyo kwenye machafuko na umwagaji damu… ni kauli ya raia anayefahamu na hapendezwi na mwenendo wa serikali” amesema Lissu.

Amesema kuwa, hata sheria ya magazeti inasema kuwa kitetendo chochote chenye lengo la kueleza ubovu wa serikali au mamlaka yake sio kosa.

“Nilichosema mimi kuwa serikali hii na matendo yaki ni ya hovyo… huyo dikitekta uchwara anahitaji kupingwa na kila mwananchi,” amesema.

“Kama wanafikiria watatutisha kwa kutuleta mahakamani, tutamkabili mahakamani na tutamkabili nje.

“Ni wakati wa wazalendo kusema kuwa, Tanzania ni nchi ya vyama vingi na ina Katiba na sheria. Katiba yetu inatambua haki za binaadamu na moja haki za binaadamu ni kueleza ujinga wa watawala wanapofanya ujinga,” amesema.

 

error: Content is protected !!