Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu, Prof. Assad wapenyeza ‘sms’ Ikulu
Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Prof. Assad wapenyeza ‘sms’ Ikulu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema
Spread the love

 

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Prof. Mussa Assad, aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wamemshauri Rais Samia Suluhu Hassan, ’kuanza upya.’ Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya Ripoti ya CAG wa sasa, Charles Kichere ya mwaka 2019/2020 kusheheni uozo uliotendwa na viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali.

Lissu na Prof. Assad kwa wakati tofauti na kutokana na uozo katika ripoti hiyo, wameshauri Rais Samia kufagia baadhi ya watendaji na wengine kuongezewa uwezi ikiwa ni hatua za kuponya taifa.

Kutokana na uchambuzi alioufanya Prof. Assad katika uzinduzi wa mfululizo wa midahalo ya umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM), tarehe 10 Aprili 2021, Lissu amesema ‘ni uchambuzi mzito na ulioshonwa vizuri.’

Kwenye uchambuzi wake, Prof, Assad alisema, asilimia 60 ya watendaji wa serikali, hawana uwezo.

“Nimemsikiliza Prof. Mussa Assad kuhusu ufisadi katika taasisi za umma. Miradi mikubwa, ndege za ATCL, SGR, Stiegler’s Gorge ni majanga yajayo ya kiuchumi. Namshauri Rais Samia kuunda Tume ya Uchunguzi kabla mambo hayajaharibika zaidi,” ameshauri Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Akizungumza kwenye midahalo huo, Prof. Assad ameshauri Rais Samia kuwaondoa watu wa namna hiyo, ili kuanza upya.

Prof. Mussa Assad, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali

“Watu wengi ni reformatting (kubadilisha) sio rebooting, kwangu mimi asilimia 60 ya watu tulionao hawafai, tuwapige chini tuanze upya. Tuanze na wale asilimia 40 wazuri kidogo.

“Lakini sababu hilo ni somo, wale ambao in the future (mbeleni) watakuwa wa ovyovyo, dawa yao tuwapige chini taunze upya,” ameshauri Prof. Assad.

Ushauri huo wa Prof. Assad umekuja wakati akizungumzia madudu yaliyoibuliwa na CAG Charles Kichere, kupitia ripoti yake aliyoiwasilisha bungeni tarehe 8 Aprili 2021.

Miongoni mwa madudu yaliibuliwa katika Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Mradi wa Kufua Umeme katika Mto Rufiji (Stigler’s Gorge).

CAG Kichere alisema, ATCL ilijiendesha kwa hasara katika kipindi cha miaka mitano mfululizo, huku bodi yake ikikosa wajumbe wenye uzoefu kuhusu mambo ya usafiri wa anga. Wakati Stigler’s Gorge ikitumia upembuzi yakinifu uliopitwa na wakati.

“Wakati niko ofisini katika vitu ambavyo niliomba, ni vitu vitatu SGR, document (nyaraka) ya ATLC mpya, project (mradi) ya Stigler’s feasibility studies, na sikupewa hata moja. Nilichopata ilikuwa barua kwamba, mwaka haujamalizika na kwa hiyo ukaguzi wa hesabu si wakati wake.

“Na kila mtu mwenye akili, alikuwa anajua ninachotaka hakikuwa ukaguzi wa hesabu, lakini (barua) ilikuwa majibu ya kiufundi ya kuniondoa katika issue ile,” amesema Prof. Assad.

Kuhusu ATCL, Prof. Assad ameshauri shirika hilo livunjwe, kisha mali zake ziuzwe, fedha zitakazopatikana zilipe madeni yake. Ili ianzishwe kampuni nyingine.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

“Ilikuwa tuuwe kwanza ATCL, ife kabisa ili wale wanaodai pesa tulipe kile tukatachokipata, kwa hiyo ndege ziuzwe, asset (mali) zote ziuzwe, kitakachopatikana walipwe watu wote ili tumalize,” ameshauri Prof. Assad na kuongeza,” alisema Prof. Assad.

Na kwamba, sasa hivi madeni yapo, na wale waliodai zamani watadai tena sababu kampuni ile ile “ukiuwa kampuni yote, madeni unayafuta halafu unaanzisha kampuni nyingine.”

Baada ya Prof. Assad kutoa ushauri huo, Lissu amemshauri Rais Samia kuunda Tume ya kuchunguza miradi hiyo, kabla mambo hayajaharibika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!