April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama yamweka Lissu njia panda

Spread the love

MAHAKAMA Kuu nchini Kanda ya Dar es Salaam, imesitisha kutoa uamuzi wa kuapishwa ama kutoapishwa kwa Mbunge Mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Jaji Sillirus Matupa amesema, atatoa uamuzi tarehe 9 Septemba 2019, na kwamba hana haraka ya kuzuia kuapishwa kwa Mtaturu.

Jaji Matupa amesema, mahakama hutoa uamuzi kwenye kesi za uchaguzi hata kama mbunge akiwa ameapishwa, hivyo haoni haja ya kuharakisha uamuzi.

Ni katika kesi ya kupinga Lissu kuvuliwa ubunge wa kwenye mahakama hiyo, iliyofunguliwa na Alute Mughwai ambaye ni kaka wa Lissu.
Leo tarehe 2 Septemba 2019, Jaji Matupa alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili – Serikali (mlalamikiwa) na ule wa mlalamikaji (Lissu) .

Jopo la mawakili 13 wa serikali liliongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Vicent Tangoh huku Upande mlalamikaji ukiongozwa na Peter Kibatala.

Miongoni mwa hoja zilizowasilishwa na Kibatala ni pamoja na mbunge akifanya kosa, atapewa onyo baada ya kusikilizwa au adhabu nyengine baada ya kusikulizwa.

Licha ya kueleza kuwa Lissu amepewa adhabu bila kusikilizwa, amedai kuwa kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza kesho tarehe 3 Septemba ambapo itakuwa siku ambayo ataapishwa Mtataru

Kutokana na hivyo, ameiomba mahakama kumzuia Spika Job Ndugai kumuapisha mbunge huyo.

Kibatala ameeleza, Mtaturu akiapishwa, maombi hayo hayatakuwa na maana .
Upande wa serikali ulijibu hoja hizo pamoja na kuzitaja aya zilizoondolewa kwenye uamuzi wa Jaji Matupa wa wiki iliyopita ambazo ni aya ya 2,5, 6(a), 9 (t) na (s) za kiapo, zimebeba maombi ikiwa tayari zimeondolewa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizaa saa nne asubuhi mpaka saa 3 usiku.

error: Content is protected !!