SALUM Mwalimu, mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ndiye amir jeshi mkuu ajaye. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).
Amesema, Lissu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, anakwenda kumshinda kwa kura nyingi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni katika Viwanja vya Shujaa, Morogoro tarehe 29 Septemba 2020 amesema, watumishi wa umma na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji wajiandaye kisaikolojia kuongozwa na Chadema.
“Chadema hatuji na askari wetu, hatuna wanajeshi wetu wala watumishi wa umma tuliowaweka pembeni, tunakuja kutumia watumishi, jeshi haohao, kinachokwenda kubadilika ni jambo moja tu, kila aliyepo kwenye nafasi yake ahakikishe anatenda haki na kutoa uhuru kwa raia tunaokwenda kuwaongoza,” amesema.
Pia amesema tayari wamempa taarifa Dk. Magufuli kwamba hawana kinyongo naye, bali watamtunzia heshima yake kama Rais Mstaafu.
Leave a comment