Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Narejea Tanzania kabla ya Julai 28
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Narejea Tanzania kabla ya Julai 28

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TUNDU Antipas Lissu, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, atarejea Tanzania mwishoni mwa mwezi huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, atafanya hivyo ili aweze kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 Julai 2020.

Mikutano hiyo, pamoja na mambo mengine, itampitisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Mchakato wa uchakuaji na urejeshaji fomu za kuwania Urais wa Tanzania unaanza leo Jumamosi tarehe 4 hadi 19,2020.

Wagombea au mawakala wao watakuwa na fursa ya kuchukua fomu kisha kutafuta wadhamini 100 katika kila kanda kumi za chama hicho.

Lissu ni miongoni mwa wanachama ambao wamekwisha tia nia hadharani ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki.

Akijojiwa na mwandishi nguli nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu katika kipindi chake kinachorushwa na JeneraliOnline, Lissu amesema, baada ya safari ndefu ya kutibu majeraha na kupona, sasa yuko tayari kurejea nchini humo.

Amesema anarejea ili kuomba ridhaa ya wana Chadema na Watanzania kumchagua kuwa Rais wa Tanzania ili kuwatumikia kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja kwani ana imani mtu mmoja pekee hawezi kuongoza nchini.

Tangu tarehe 7 Septemba 2017, Lissu aliposhambuliwa na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake Area D jijini Dodoma, mwanasiasa huyo amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu.

Siku hiyohiyo usiku, alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hadi tarehe 6 Januari 2018 alipopelekwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Lissu mwenyewe amekwisha kusema amepona na hatumii dawa zozote na anachosubiri ni kureja nyumbani Tanzania kuendelea na shughuli zake mbalimbali hasa za kisiasa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!