Sunday , 5 February 2023
Home Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu Lissu, amesema safari ya miaka 30 ya vyama vingi nchini Tanzania haikuwa rahisi bali misukosuko mingi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Lissu amewapongeza viongozi wa chama chake na wanachama kwa kufikia hatua waliyopo sasa licha ya misukosuko mingi.

Lissu ambaye amewasili leo Jumatano tarehe 25 Januari 2023 nchini akitokea Ubelgiji alikokuwa akiishi kwa takribani miaka sita,  ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Buliaga uliopo Tekeme jijini Dar es Salaam.

“Safari ya miaka 30 ya Tanzania kama nchi ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru bali kwa miba kwa mawe na kuna damu umemwagika watu wamekufa wengine wamepotea tumeumizwa sana wote. Kama tumefika hapa tunastahili kupongezana,” amesema Lissu.

“Huu ni mwaka wetu wa thelathini kama chama cha siasa kwahiyo naomba nichukue fursa hii nikupongeze Mwenyekiti viongozi wanachma na wote waliotuunga mkono katika shida zote hizi na misukosuko,” ameongeza

error: Content is protected !!