August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu mbaroni

Spread the love

TUNDU Lissu Mbunge wa Singida Mashariki ametiwa mbaroni na jeshi la Polisi Mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara, anaandika mwandishi wetu.

Taarifa zinasema kuwa Lissu alikamatwa mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo katika Jimbo lake eneo la Ikungi mkoani humo.

Chanzo cha habari hizi kinaeleza kuwa Lissu alikamatwa  na Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai wa jeshi hilo aliyejitambulisha kama Babu Mollel kwa maelekezo ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Singida na kwamba maelekezo hayo yanatoka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema kuwa Lissu usiku huu anaweza kusafirishwa hadi Jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema kuwa Lissu amekatwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi Jana Tarehe 2 Agosti mara baada ya kutoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akizungumza na wafuasi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema).

Mtandao huu utakujuza kila kinachoendelea..

error: Content is protected !!