Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kurejea jukwaani leo
Habari za Siasa

Lissu kurejea jukwaani leo

Spread the love

TUNDU Antiphas Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020 ataanza tena kampeni za kuwania urais wa nchi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Jana Ijumaa, Lissu anamaliza kutumikia adhabu ya siku saba ya kutokufanya kampeni baada ya kufungiwa na Kamati ya Kitaifa ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Adhabu hiyo ilitolewa tarehe 2 Oktoba 2020 baada ya malalamiko kutolewa na vyama viwili vya NRA na CCM kwamba Lissu, ametoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika.

Tumain Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema amesema, kesho Lissu ataendelea na kampeni zake Mkoa wa Dodoma na kumalizia Singida.

Jumapili, Lissu ataendelea na mikutano ya kampeni mkoani Singida na Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 atakuwa mikoa ya Tabora na Shinyanga.

Katika kipindi hiko cha adhabu, Lissu alibadilishiwa majukumu na Kamati Kuu ya Chadema ya kuanza kufanya shughuli za kijamii kwa kofia ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Bara.

Miongoni mwa shughuli hizo, Lissu alikwenda soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam akitumia usafari wa mabasi ya mwendokasi ambako alinunua mahitaji mbalimbali ikiwemo matunda na mchele.

Jana Alhamisi, Lissu alikwenda Mlimani City jijini humo na Manzese ambako nako alifanya mahemezi kama mbalimbali ikiwemo kununua nguo kwa wafanyabiashara ndogondogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!