September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu funga kazi, polisi watweta

Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki amefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam kwa mahojiano, polisi wamekuwa na kazi ya ziada, anaandika Shaban Matutu.

Idadi ya polisi kwenye kituo hicho imeongezwa wakati alipofikishwa huku shughuli nyingine ndani ya kituo hicho zikionekana kusimama.

Awali, Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chadema hakua akijulikana alipo kutokana na polisi kutotoa taarifa kamili baada ya kumkamata jana jioni.

Lissu amefikishwa kwenye kituo hicho leo saa 7:54 mchana na gari aina ya Land Cruser lenye namba za usajili T 312 CWM akiwa chini ya ulinzi mkali.

Amefikishwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya mahojiano kutokana na madai ya kutoa kauli ya kichochezi ‘dikteta uchwara’ juzi wakati akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipoenda kusikiliza kesi ya uchochezi iliyohusu kauli yake ya awali ya ‘dikteta uchwara’.

Wakati Lissu akifikishwa eneo la kituo hicho, polisi walikuwa wamezunguka eneo hilo huku kukiwa na  ulinzi mkali pamoja na silaha za moto.

Askari waliokuwa eneo hilo walikuwa wakiwaondoa wananchi na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia matukio katika eneo hilo.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa alifika kituoni hapo saa kumi kasoro, hata hivyo alizuiwa kuingia ndani.

Saa 4:02 Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam kituoni hapo na gari lenye namba za usajili SM 10584 ambapo aliruhusiwa kuingia ndani kumuona Lissu ambaye anahojiwa.

Lissu bado anaendelea hojiwa…

error: Content is protected !!