June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu azungumzia kukamatwa, tuhuma za Mbowe

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

MAKAMU mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanania cha Chadema, Tundu Lissu amesema, tukio la kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ni vita ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ameyasema hayo leo Ijumaa, tarehe 23 Julai 2021, akizungumza na wanahabari kwa njia ya mtandao, kuhusu tukio la kukamatwa kwa Mbowe na wenzake 11.

Mbowe na wenzake, walikamatwa saa 8 za usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, wakiwa katika Hotel ya Kingdom jijini Mwanza, walipokuwa wamekwenda katika kongamano la kudai katiba mpya.

Wakati wenzake 11 wakipelekwa kituo kikuu cha polisi Mwanza, Mbowe alisafirishwa hadi Dar es Salaam alikohojiwa kwa tuhuma za kupanga njama za mauaji ya viongozi na ugaidi.

Lissu amesema “kukamatwa kwa mwenyekiti Freeman Mbowe ni vita ya kisiasa na kwa vile ni vita ya kisiasa, matokeo yake itakuwa kama ya miaka yote, hawana hatia. Hili nafikiri ni vizuri tukalielewa hivyo.”

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

“Hili kosa jipya linalosemwa na polisi la ugaidi ni mojawapo na ni sehemu ya mlolongo mrefu wa makosa ya kubambika ya jinai, ambayo mwenyekiti Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema wamefunguliwa katika vipindi mbalimbali,” asema Lisuu aliyehi nchini Ubelgiji.

Lissu amesema, “kwa sababu tu ya kuwa viongozi na wanachama wa upinzani, ni molongo tu wa vita dhidi ya Chadema ambayo imeendeshwa na CCM.”

Lissu amedai, hatua ya Mbowe kutuhumiwa kwa makosa ya ugaidi, imelenga kusitisha harakati za kudai katiba mpya.

“Mbowe amekamatwa na kupewa makosa ya ugaidi ili anyimwe dhamana, kwa ajili ya kukwamisha mchakato wa kudai katiba mpya, hadi sasa hatujui mwenyekiti atafikishwa lini mahakamani,” amedai Lissu.

error: Content is protected !!