Wednesday , 29 March 2023
Habari za Siasa

Lissu azuiwa Same

Spread the love

WANANCHI wa Hedaru, Same mkoani Kilimanjaro, wamezuia msafara wa Tundu Lissu, mgombea urasi wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Taarifa kutoka eneo hilo zinaeleza, wakazi wa eneo hilo walikuwa na taarifa za Lissu kupita akirejea Dar es Salaam baada ya kuamliza awa mu ya pili ya kampeni zake za urais.

Baada ya wananchi hao kujiridhisha kwamba Lissu yupo njiani kurejea Dar es Salaam, waliitana na kuanza kujipanga huku wakiimba.

Na kwamba, Lissu hakuwa na taarifa ya kuwepo kundi kubwa la wananchi wakimsubiri Hedaru.

Mara baada ya msafara wake kutokea, wananchi hao walisimama barabarani huku wakiimba Lissu, Lissu, Lissu…

Mgombea huyo alisimama eneo hilo na kuwapungia mkono huku akiashiria kuondoka.

Hata hivyo, wananchi hao walizuia gari lake wakimtaka azungumze chochote.

Ndipo Lissu alipolazimika kuchukua kipaza sauti na kuzungumza na wananchi hao hao kwa uchache.

Alianza kwa kuwasalimia kisha akasema “Ninakwenda Dar es Salaam lakini nitakuja kufanya mkutano hapa katika awamu ya tatu.”

Baada ya kutamka maneno hayo, wananchi hao walipiga kelele kufurahia na kisha mmoja mmoja alianza kuondoka mbele ya gari lake ambapo lilikuwa limeambatana na magari mengine ya msafara na kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

2 Comments

  • Absolutely I like the way he deliver his Message to people. He is very very Courageous, full self confidence. And I dont know if the CCM Government has noticed that Tindu Lissu has the highest acceptance to peoople?
    We Tanzanians let us continue to pray for thi gue so that God will make him Successful.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!