Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu azidi kusota polisi Dar
Habari za SiasaTangulizi

Lissu azidi kusota polisi Dar

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema (wakwanza) kulia ni Wakili Fatma Karume, Mwanasheria wa kujitegemea
Spread the love

JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam limetakiwa kumfikisha Mahakamani, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, badala ya kuendelea kumuweka Mahabusu, anaandika Hamisi Mguta.

Lissu ambaye pia ni  Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alikamatwa jana jijini Dar es Salaam akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi ambapo alikuwa akielekea jijini Kigali, Rwanda kuhudhuria kikao cha halmashauri ya vyama vya wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) kilichoanza leo..

Kauli ya kutaka Lissu afikishwe mahakamani imetolewa leo na Fatma Karume, Mwanasheria wa Tundu Lissu alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada kutoka kituo kikuu cha Polisi, kanda maalum ya Dar es Salaam ambapo Tundu Lissu alikuwa akihojiwa baada ya kukamatwa na kulala mahabusu.

“Tumeamua, tutalipeleka jeshi la polisi Mahakamani kuiomba mahakama iiambie jeshi la polisi imlete mahakamani jumatatu ili kama wana kesi waendelee na kumkabidhi Tundu Lissu kwa mahakama, wamuachie au wamapeleke mahakamani,” amesema.

Wakili Fatma amesema hakuna sababu yoyote ya kumnyima dhamana Lissu na kuwa jeshi la polisi halijasema kama Lissu amefanya uchochezi kwa nani na alichochea afanye jambo gani.

“Nilimuuliza ndani kwamba Tundu Lissu mtampeleka mahakamani lini wakaniambia hawajui na bado wanaendelea kufanya upelelezi, ina maana nchi hii tunakamata kwanza kisha upelelezi baadaye?,” alihoji.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Polisi wamemchukua Lissu kutoka kitoani hapo kuelekea naye nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa ambapo hadi Mtandao huu unapata taarifa hizo haijulikani upekuzi huo ulihusu kitu gani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!