Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu awaburuza kortini Ndugai na Mkuchika
Habari za Siasa

Lissu awaburuza kortini Ndugai na Mkuchika

Tundu Lissu, Rais wa TLS
Spread the love
MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amepeleka ombi katika Mahakama  Kuu Kanda ya Dodoma, akiomba kumshtaki Job Ndugai, Spika wa Bunge na George Mkuchika, mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Haki, Kinga  na Madaraka ya Bunge, anaandika Dany Tibason.
Lissu anaomba kuwashtaki Ndugai na Mkuchika kwa kuwafungia kuhudhuria vikao vya Bunge wabunge watatu wa Chadema ambao ni Halima Mdee (Kawe), John Mnyika wa Kibamba na Ester Bulaya wa Bunda.
“Tumepeleka maombi ili Mahakama Kuu ili iweze kutoa amri ya kufutilia mbali uamuzi wa Spika wa Bunge letu wa kumsimamisha  Mnyika kwa vikao saba vya bunge hili la saba.
Pia tunaiomba mahakama ifute uamuzi wa Bunge wa kuwasimamisha  Mdee na Bulaya kuhudhuria vikao vilivyobaki vya Bunge hili na vikao vya Bunge la nane na Bunge la tisa,” amesema.
Amewaeleza wanahabari leo mjini Dodoma kuwa uamuzi wa Spika ulikuwa na upendeleo kwani uliwanyima haki wabunge wa upinzani kwa manufaa ya serikali na chama taewala.
“Tumeenda mahakamani ili pia tuweze kujua je mamlaka ya Bunge ya kumsimamisha Mbunge yana ukomo, je Bunge linaweza likaamua likamsimamisha Mbunge kwa vikao vyote ishirini?”
Katika mkutano huo na wanahabri, John Heche, John Heche alieleza kuwa jeshi la polisi linamuwinda ili kumkamata kwa tuhuma za uchochezi kufuatia hamasa aliyoitoa kwa wananchi wa jimbo lake kuwa wazuie wizi wa rasilimali unaoendelea.
“Nasema kwa kurudia tena, nipo tayari kukamatwa na nitatoka nje ya ukumbi wa Bunge, waje tu kunikamata, siogopi kitu wala mtu yoyote.
“Mimi nimetumwa na wananchi nije niwasemee hapa na narudia tena, kama Rais amesema watu wa Acacia ni wezibasi wananchi wa Tarime wana haki ya kuwakamata wezi hao katika maeneo yao,” amesisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!