July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu atua Kenya kuzindua kitabu chake

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema

Spread the love

 

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrais na Maendeleo (Chadema), yupo nchini Kenya kwa maandalizi ya uzinduzi wa kitabu chake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, Profesa George Wajackoya wakati akizungumza na mtandao wa Nation Africa leo tarehe 24 Juni 2021, Lissu atazindua kitabu chake ‘Vivuli- Bunge na Uwajibikaji kwa Afrika Mashariki’ Ijumaa tarehe 25 Juni 2021.

Prof. Wajackoya amesema “ni kweli (Lissu) yupo nchini (Kenya) kwa ajili ya kuzindua kitabu chake katika Hoteli ya Windsor.”

Lissu ametua Kenya akitokea Ubelgiji alikokwenda baada ya uchaguzi mkuu 2020. Kwenye uchaguzi huo, alikuwa mgombea urais Tanzania Bara kupitia Chadema.

Awali, Lissu alikwenda Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi jijini Dodoma mwaka 2017, kutokana na shambulizi hilo, amefanyiwa operesheni mara 25.

error: Content is protected !!