January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu aponda Baraza la Mawaziri

Spread the love

MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu na mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameuponda uteuzi wa baraza la Mawaziri uliofanywana Rais John Magufuli kwa madai kuwa Mawaziri ni wale wale na sura ni zile zile. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na Mwanahalisi Online Lissu alisema kuwa uteuziwa Rais hauwezi kuwa na kasi ile ile ambayo watanzania wanaitegemea kutokanana kuwa zaidi ya Mawaziri 11 walikuwa katika baraza lile la Kumi.

Mbali na kuliponda Baraza hilo amesema anashangazwa  na Rais Kumteua Sospeter Muhango ambaye alifukuzwa na Bunge wakati wa bunge lililopita kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

Lissu amesema kitendo cha Magufuli kumteua Muhongo kuwa katika Wizara ile ile ambayo bunge lilimfukuza kutokana na kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha unajenga mashaka na unatia wasiwasi ni vigezo gani vimetumika kumteua tena.

Amesema ni aibu kwa Rais kumteua mtu ambaye kimsingi alifukuzwa na wabunge kutokana na wizi wa mabilioni ya fedha jambo ambalo linaonesha wazi kuwa hakuna jambo jipya zaidi ambalo litafanyika kutokana na kuteua watu ambao kimsingi walikuwa na kashfa.

“Hapa nimaona rais kalifanya bunge lijalo kuwa la moto zaidi kwa kuwa ametuletea majizi ambao bunge lilisha wafukuza hatujaelewa katumia vigezo gani hayo inaonesha wazi  kwamba kuna kila sababu ya kujiuliza kuna sili gani Ikulu kwa hatua ya kuwateua watu ambao wanatuhuma,” amesema Lissu.

Naye askofu wa Kanisa la Tanzania Methodisti  jimbo la Dodoma Joseph Bundara alisema hatuaya Magufuli kuteua baraza dogo linawatia moyo watanzania kwa kutambua wazi kuwa itasaidia kubana matumizi ambayo yalikuwa yakifanywa.

Amesema licha ya kuwepo baadhi ya Mawaziri waliokuwa na tuhuma lakini wakibanwa vyema wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa ajili ya kutumia rasilimali za nchi kutumiwa na watanzania wote tofauti na ilivyo sasa.

Naye Mwenyekiti wa wanataaluma wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania Poul Loisulie, alisema kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuwateua mawaziri wote kwa kukamilisha baraza la Mawaziri kunaweza kuwa kunatokana na kuwepo kwa sintofahamu katika uchaguzi wa Zanzibar.

Amesema kuna uwezekano Wizara ambazo hazijapata Mawaziri ni kutokana na Rais kushindwa kuwapata watu wanaofaha huku pakiwepo na uwezekano wa kuacha nafasi kutoka Zanzibari.

Hata hivyo alisema jambo pekee ambalo Magufuli anatakiwa kusifiwa ni kuwateua watu ambao hawakuwa katika mtandao na wala hawakudhaniwa kama wangeweza kuteuliwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia nafasi za uwaziri.

error: Content is protected !!