August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu ‘ampasua’ Magufuli

Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki amesema, mwenye mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa ni Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) pekee, anaandika Faki Sosi.

Amesema, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa mwongozo huo na si vinginevyo na kwamba, rais hana mamlaka ya kusema au kufanya lolote kuhusu mikutano ya hadhara.

Lissu ametoa kauli hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kutoka kusikiliza kesi anayotuhumiwa kwa uchochezi uliotokana na kauli yake ya ‘Dikteta Uchwara.’

Hivi karibuni Rais John Magufuli amesema kuwa, mikutano ya kisiasa ifanywe na wabunge na madiwani wa eneo husika.

Akiwa katika viwanja vya mahakama Lissu “ukitaka kujua huu ni dekteta uchurwa, ni pamoja na kauli ya kutaka watu wafanye mikutano kwenye maeneo yao.

“Sheria ya Tanzania inasema kuwa, chama chochote kilichosajiliwa usajili wa kudumu, kina haki ya kufanya mkutano wa hadhara  mahala popote nchini isipokua kwenye kambi za  majeshi, hasomi sheria, anachofikiria kichwani kwake sio sheria,’’  amesema Lissu.

Amesisitiza kuwa, mikutano ya hadhara iliyopangwa kufanyikia tarehe 1 Septemba mwaka huu itaendelea na kwamba, kuwa na kesi mahakamani haizuii kufanya siasa.

“Tuna haki kama alivyo na haki Rais John  Magufuli na ole Sendeka, mahakamana itakapotuambia kuwa acheni, pengine tutaacha,” amesema Lissu.

Katika kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu amesema, Lissu amesomewa maelezo ya awali na Bernard Kongola, Wakili Mkuu wa Serikali  mbele ya Hakimu Yohana Yongola kwamba, anatuhumiwa kwa tuhuma za kauli za uchochezi.

Kongola amedai kuwa, Lissu alitenda kosa la kutoa kauli ya uchochezi kwenye viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai, Lisuu alikamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake Tegeta na kuwa baada ya kuhojiwa, alikiri kuwa ametenda kosa.

Lissu amekiri kuwa, anatuhumiwa lakini amekana kutamka maneno ya uchochezi, pia amekanusha kuwa alikiri baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi nyumbani kwake.

Hakimu Yongola amesema kuwa, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 24 Agosti mwaka huu.

 

 

 

error: Content is protected !!