Monday , 4 March 2024
Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Kinana

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema mazungumzo ya maridhiano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chadema yamevunjika kutokana na CCM kutokubali mapendekezo yao hususan madai ya upatikanaji katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, leo tarehe 6 Februari 2024 kwa njia ya simu, Lissu amesema si kweli kwamba mazungumzo hayo yamevunjika kutokana na Chadema kutumia kauli za udhalilishaji katika mikutano yake ya hadhara.

Lissu ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, kusema mazungumzo hayo yamevunjika baada ya Chadema kutumia mikutano ya hadhara kukashifu na kudhalilisha viongozi wa Serikali hasa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Hilo la kumdhalilisha Rais halijawahi kuwa hoja ya mazungumzo ya maridhiano. Tulichokizungumzia na walichokikataa ni mabadiliko ya Katiba na mfumo mpya wa uchaguzi. Hatujawahi kuzungumzia kauli na msimamo wetu kuhusu Rais Samia na utendaji kazi wake. Wanataka kubadilisha ‘narrative’, amesema Lissu na kuongeza:

“Suala sio kutuita tena kwenye meza ya mazungumzo. Suala ni je, wako tayari kukubaliana na mapendekezo yetu juu ya Katiba Mpya na mfumo mpya wa uchaguzi? Kama hawako tayari kufanya hivyo, mazungumzo hayatakuwa na maana yoyote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!