April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu amchongea Ndugai ughaibuni

Spread the love
BUNGE la Jamhuri ya Muungano, limeanza kuchunguzwa rasmi na Umoja wa Mabunge ulimwenguni (IPU), kufuatia kufunguliwa mashitaka rasmi na aliyekuwa mbunge wa upinzani nchini, Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na umoja huo wenye makazi yake Geneva, nchini Uswiswi, Bunge la Tanzania, sasa linalazimika kujibu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, zilizowasilishwa na Lissu kwenye Bunge la IPU.

Kamati inamuomba Katibu Mkuu wa IPU kuwasilisha uamuzi huu kwa mamlaka ya kibunge ya Tanzania na kuomba ruhusa ya kutembelea Tanzania kama ilivyopendekezwa.

Mbali na Bunge hilo kufanyia kazi uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli; na tayari Kamati ya Haki za Binadamu imepanga kuwasili nchini, kuchunguza tuhuma hizo.

Bunge la Tanzania, ni mwanachama wa IPU na hivyo linawajibika kuheshimu na kuzingatia haki za wabunge wake kwa mujibu wa sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu na za wabunge.

Katika taarifa yake ya mwishoni mwa wiki, Kamati ya IPU imesema, imesikitishwa na jaribio la mauaji dhidi ya Lissu na vitisho vilivyokuwa vinatolewa dhidi yake; kuondolewa kwa walinzi wa katika makazi yake, muda mfupi kabla ya shambulio hilo.

Kamati imeomba kupatiwa maelezo rasmi na ya kina kuhusu waliohusika na shambulio hilo na wale waliowatuma, ikiwamo na kupotezwa kwa kamera za CCTV kutoka kwenye jengo la makazi ya Lissu.

“Kamati imesisitiza kwamba vitisho dhidi ya maisha na usalama wa Wabunge, vikiachwa bila kuadhibiwa, sio tu vinakiuka haki ya kuishi, ya kuwa salama na ya uhuru wa mawazo ya Wabunge, bali pia inaathiri uwezo wa Bunge kama taasisi kutekeleza wajibu wake,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa imesema: “Kamati imesikitishwa kufahamu kwamba Lissu alikamatwa na polisi mara kadhaa, na kwamba bado anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya jinai yanayoenda kinyume na haki zake za msingi za binadamu, na inapenda kupata maelezo rasmi kuhusu misingi ya kiushahidi na ya kisheria ya kila mojawapo ya mashtaka hayo.

“Kamati inatambua kwamba ninataka kurudi Tanzania haraka iwezekanavyo, na inapendekeza kuwa ujumbe wa Kamati unisindikize wakati nitakaporudi, kwa imani kwamba kutembelea Tanzania kutatoa fursa ya kukutana na mamlaka za kiserikali, kibunge na kimahakama, pamoja na wadau wengine, ili kuiwezesha Kamati kuelewa suala hili vizuri zaidi.”

IPU imechunguza maamuzi ya kuwafukuza au kuwasimamisha Wabunge kuhudhuria vikao vya Bunge, vitendo ambavyo vimekithiri sana katika Bunge letu.

error: Content is protected !!