TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, amekamilisha hatua za mwisho za ujazaji fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Lissu akiambatana na mgombea mwenza, Salum Mwalimu, wamefika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kisheria ya ujazaji wa fomu zao za kugombea.
Akizungumza baada ya kukamilisha hatua hiyo, Lissu amesema wamefika katika mahakama hiyo kula kiapo cha ujazaji wa fomu hizo.
“Mimi ni mteule wa Chadema kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Salum anagombea makamo wa rais, taratibu ya sheria ya uchaguzi baada ya kutafuta wadhamini.”

“Kinachofuata ule kiapo mbele ya Jaji Mkuu, ukija kula kiapo kama sehemu ya kukamilisha ujazaji fomu ya uteuzi wa kugombea kinachofuata ni safari ya Dodoma kuwasiliha fomu za uteuzi siku ya Jumanne,” amesema Lissu.
Uteuzi wa wagombea urais itafanyika tarehe 25 Agosti 2020 Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.
Baada ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Leave a comment