Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aijibu NEC ‘ngoma hii hawaiwezi’
Habari za SiasaTangulizi

Lissu aijibu NEC ‘ngoma hii hawaiwezi’

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameeleza kupuuza kauli iliyotolewa na Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Akijibu kauli ya Dk. Mahera mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 30 Septemba 2020, jijini Arusha Lissu amesema kauli ya mkurugenzi huyo ni ya kutaka kuvuruga uchaguzi.

“Na sisi tumefanya kama Magufuli (Dk. John Magufuli, mgombea urais kupitia CCM) kukuta na watu barabarani. Huu ni msimu wa mikusanyiko, kuzungumza na wananchi na hii hawaitaki, Magufuli ni ruhusa lakini Tundu Lisu si ruhusa.

“Kilicho halali kwa Magufuli ni halali kwa Tundu Lisu, Magufuli ni mgombea na Lissu ni mgombea. Kilicho halali kwa CCM ni halali kwa Chadema,” amesema Lissu.

Jana tarehe 29 Septemba 2020, akizungumzia masuala ya mwendelezo wa kampeni Dk. Mahera alisema”tumevumilia sana, na IGP amevumilia sana, kuanzia sasa mtashangaa watu watapigwa mabomu kule ambako wameambiwa waache kwenda na polisi, nadhani mliona jana wamepigwa mabomu kule Nyamongo’’

Kutokana na kauli hiyo, Lissu amesema urataribu wa kutishiana kupiga watu mabomu ni kutaka kuvuruga uchaguzi, huku akisisitiza pale chama ama mgombea ana malalamiko na mgombea mwenzake, anapasa kwenda kwenye tume ya maadili na si kupiga mabomu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

“Kwa hiyo, huu urataribu wa kupigana mabomu, wa kutishiana kupiga watu mabomu ni kutaka kuvuruga uchaguzi, kwa sababu wanaona kabisa wanashindwa ndio maana wameingia taharuki. Ni dalili wazi za kuonesha kwamba, hii ngoma hawaiwezi,” amesema Lissu na kuongeza:

“Kama kuna mtu anayekiuka maadili, kanuni hizi hazijasema apigwe mabomu. Kanuni hizi zimesema kama kuna mtu ambaye hapendezwi na jambo lolote linalofanywa na chama chochote au mgombea yeyote au na tume au na serikali au watendaji wake, basi huyo asiyeridhika aende kwenye kamati ya maadili ya ngazi husika.”

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho amesema, ratiba yao waliipanga kwa ajili ya kutumia Helikopta, hata hivyo walikataliwa na hivyo kuamua kutumia magari kwa ajili ya kukamilisha ratiba hiyo.

Na kwamba, matumizi ya magari kwao yamekuwa na ufanisi mkubwa kuliko kama wangetumia Helikopta kwa kuwa, matumizi ya magari yamesababisha kukutana na watu wengi zaidi ya walivyotarajia.

“…tukasema tutatumia magari, ile ratiba ya Helikopta tumeifanya kwa magari na tumeitekeleza kwa ufanisi hata tofauti na tulivyotarajia sisi, tumeona watu wengi barabarani kuliko tungetumia Helikopta,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!