April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu aichokonoa ATCL, ashusha hoja zake

ATCL Dreamliner

Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, amehoji faida halisi inayotokana na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), tangu Rais John Magufuli aingie madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo tarehe 30 Oktoba 2019, Lissu amesema, kuna haja ya kuangalia upya uendeshaji hilo liingize faida.

“Hadi sasa Magufuli (Rais) kanunua ndege 7 sawa na matumizi ya Sh. 1.769 trilioni, na kuingiza Bil 30 tu kama faida ndani ya ATCL, kwa nini hatuoni kuna haja ya kuangalia namna ya kufanya biashara hii upya,” amedai Lissu.

https://twitter.com/tundu_lissu/status/1189586737611395073?s=21

Kwenye andishi hilo amehoji,  kwanini wataalamu wa masuala ya uchumi wameruhusu serikali kutumia Sh 1.7 Trilioni, kununua ndege katika kipindi cha miaka mitatu, wakati uwekezaji huo hautaleta faida mapema.

“Wachumi mnaruhusu vipi kutoa Tril 1.769 ndani ya miaka 3, zisizo kuwa na matarajio ya kurudi leo au kesho? ” amehoji Lissu.

Wakati huo huo, Lissu amehoji, ndege hizo zinanunuliwa kwa masilahi ya mtu mmoja au kwa ajili ya kufanya biashara? Na kueleza, fedha hizo zingesaidia kuboresha afya, elimu, miundombinu na kutoa ajira.

error: Content is protected !!