August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu afunguka kuhusu miswada ya madini

Kulia Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Sheria na Katiba. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki

Spread the love

KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni imesema miswada mitatu ya kulinda rasilimali iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni na Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Sheria na Katiba ina mapungufu yanayoweza kuliingiza Taifa katika mgogoro, anaandika Mwandishi Wetu.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Cecilia Pareso, Mbunge wa Viti Maalumu kwa niaba ya Lissu, ameeleza kuwa Sheria za Madini zilipitishwa kwa hati ya dharura mwaka 1997 na 1998, Serikali ya Tanzania iliamua kugawa bure rasilimali za Taifa.

“Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 ilimpa Waziri wa kusaini mikataba ya uendelezaji madini na kuingilia hata sekta ambazo hazihusiani na madini. Mikataba hii imezipa kinga kubwa kampuni za madini ambazo ikiwa ni pamoja na kuzuia kutumika kwa sheria mpya zinazotungwa baada ya mikataba yao kusainiwa.

“Aidha, migogoro yote kati ya Serikali na kampuni hizi inaamuliwa na mabaraza ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya wawekezaji kama na si mahakama za ndani ya Tanzania,” amesema.

Aidha Pareso ameasema Muswada wa Sheria ya Maliasili na Rasilimali ya 2017 kifungu cha 2 kinatamka kuwa sheria hii itatumika Tanzania Bara pekee rasilimali kama mafuta, gesi na madini ni miongoni mwa mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

“Pia Kifungu cha 5 (2) cha muswada huu kimeweka umiliki wa rasilimali na maliasili za nchi mikononi mwa Rais kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kifungu hatari kinachoweza kuleta madhara kwa taifa.

“Mamlaka haya ni makubwa sana na yenye athari chanya au hasi pale yanapotumiwa vibaya. Endapo binadamu huyu aliyepewa cheo kikubwa hivi akiyatumia madaraka yake vibaya anaweza kuleta hatari kubwa katika taifa,” amesema.

Pareso ameitaka serikali kutengeneza kutengeneza mifumo thabiti ya kuwajenga na kuwawezesha wawekezaji wazawa kuwekeza katika sekta ya madini na gesi badala ya mfumo wa sasa ambao makampuni makubwa kwenye sekta ya madini, mafuta, gesi, na maliasili ya wanyamapori yanamilikiwa na wageni.

error: Content is protected !!