May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu afanyiwa upasuaji wa 25

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji

Spread the love

 

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, nchini Tanzania, amefanyiwa upasuaji wa 25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni mwendelezo wa matibabu anayoyapata tangu aliposhambuliwa kwa risasa zadi ya 30 huku 16 zikimpata mwilini, mchana wa tarehe 7 Septemba 2017, akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma.

Alikutana na makasa huo, wakati akitoka kuhudhuria mkutano wa Bunge uliokuwa ukiendelea.

Mara baada ya kushambuliwa, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali kisha, usiku wa siku hiyohiyo, alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Alipata matibabu Nairobi hadi tarehe 6 Januari 2018, alihamishiwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi.

Jana Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, Lissu alitumia ukurasa wake wa Twitter aliweka picha na kuandika “nimefanyiwa upasuaji wa 25.”

error: Content is protected !!