Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aeleza kitakachomrejesha Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Lissu aeleza kitakachomrejesha Tanzania

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema chama hicho kikitengeneza utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kudai katiba mpya, atarejea nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, tarehe 1 Julai 2021, akizungumza kwa njia ya mtandao, katika uzinduzi wa kongamano la kudai katiba mpya, lililofanyika kwenye ukumbi wa Baracuda, Tabata jijini Dar es Salaam.

Mwanaaiasa huyo aliyeko nchini Ubelgiji amesema, chama hicho kikitaka katiba mpya ipatikane, lazima kishirikishe wananchi.

“Tuwaandae wananchi kwenye mikutano ya hadhara na mimi niwaahidi, tukitengeneza utaratibu wa mikutano ya hadhara, nakuja Tanzania. Nitakuja Tanzania kufanya mikutano ya hadhara, sio kuja kujifungia chumbani na kukaa kwenye vikao vya ndani. Tujiandae kwenda kwa wananchi tutapata katiba mpya,” amesema Lissu.

Awali, akizindua kongamano hilo, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, aliwaagiza viongozi wa chama hicho wajiandae kufanya mikutano ya siasa.

“Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda.

Hatuko tayari kumpa Mama Samia muda, na natoa agizo kwa viongozi wote wa chama nchi nzima wajiandae mapema kwa ajili ya mikutano ya hadhara, siku ambsyo tutaitangaza,” alisema Mbowe.

Wakati huo huo, Lissu amekishauri chama hicho, kihoji makundi mbalimbali juu ya misimamo yake kuhusu upatikanaji katiba mpya.

“Sasa tunajiandaaje, Rais Samia alikutana na maaskofu juzi juzi, tuwaombe maaskofu na sisi tukutane nao tuwaambie wachague upande, tujue kama wanataka upande wa katiba ya wananchi. tuwaendee Mashekhe wetu tuwaambie wachague upande, tuendelee na utawala huu au wanataka katiba mpya,” amesema Lissu.

Mwanasiasa huyo ameongeza”tuendelee kwa taasisi zote tuwaambie wachague upande, wanachagua utawala uliopo au wanaunga mkono katiba ya wananchi. tusiwe na watu tusiojua misimamo yake.”

1 Comment

  • Asante ndugu lissu lakini acha tabia ya kuchuza watu unajaribu kukaanga mbuyu uwachie wenye meno watafune lissu mtu mwenyewe akili timamu hataweza kusikiliza porojo yako potofu lissu uelewe hawao wabaguzi walangi iko siku watakufuza bira kufunga vilago na uko mwaka nafs yako itachoka kustamili and vitendo vya ubaguzi utaondoka hapo ulippo bira kuaga wewe sio mtu mweusi wa kwanza kuona wazungu watu wamana sana lakini matokeo yake ni majuto uwelewe mzungu hamp samani mtu mweusi mpaka mwisho wa dunia kama wewe unaona wanakuthamini wanakundaganya tu jalibu kutembea mitaani hapo utaona watu waliokosa rangi wanavyo baguriwa nahata kunyanyaswa sababu ni kukosa usione anavyo sifiwa lukaku wanamsifu japo kakosa kwa faida yao kwa maana io hata wewe lissu wanaweza kukusifu kwa faida yao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!