Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aahidi neema wanafunzi elimu ya juu
Habari za Siasa

Lissu aahidi neema wanafunzi elimu ya juu

Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu amesema, akichaguliwa kuwa Rais wan chi hiyo ataondoa ubaguzi wa utoaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kupunguza riba wanayolipa kwa sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Lissu ametoa ahadi hiyo leo Jumamosi tarehe 26 Septemba 2020 alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Mwanza kabla ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Mwanza na Mkoa wa Mara.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 ukihusisha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.

“Hili suala la bodi ya mikopo ya wanafunzi, ilipoanzishwa sheria ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, kiwango cha riba kilichowekwa ilikuwa asilimia tatu ya marejesho ya mkopo.”

“Sasa wameondoa asilimia tatu na kupeleka asilimia 15. Sisi tumesema tutarudi katika mkataba wa mwanzo wa asilimia tatu ukipata ajira na kama huna ajira utalipaje hela kwani huna hela,” amesema Lissu

“Wapate ajira na tutakata watape ajira ndani na nje ya nchi ili walipe kwa asilimia tatu na tutaondoa ubaguzi kabisa katika utoaji wa mikopo.”

Lissu amesema “kwa sasa ukisoma shule binafsi hupati mkopo, kila Mtanzania ni mlipa kodi na kila Mtanzania akipata kusoma ndani na nje ya Tanzania ana stahili kupata mkopo. Tutaondoa huo ubaguzi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!