Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: 28 Oktoba siku ya ukombozi, tutashinda kwa kimbunga
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: 28 Oktoba siku ya ukombozi, tutashinda kwa kimbunga

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kupiga kura za mafuriko ili kumwezesha kushinda kwa kishindo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza …(endelea).

Pia, ameyaomba majeshi ya ulinzi na usalama kutokukubali klutumika bali waendelee kulinda amani ya nchi kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Lissu ametoa wito huo leo Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020 katika mkutano wake wa mwisho kwa leo Jimbo la Nyamagama jijini Mwanza uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

“Mwanza… tarehe 28 Oktoba 2020 tukapige kura ya mafuriko kama haya ya leo, tukapige kura ya kibunga, mkipiga kidogo wataiba, tukiwashinda robo watatuhujumu, tukipiga kwa wingi hawawezi,” amesema Lissu.

“Wazee kwa vijana, shangazi kwa wajomba na wote tukafanye hiki ambacho kitatuondoa katika utawala huu ambao unatutia umasikini, 28 Oktoba 2020 iwe tarehe ya kila mmoja kuifanya ya ukombozi.”

“Tukapige kura ya kimbuga, ili askari wetu, mwalimu wetu, mkulima wetu, mfanyakazi wetu, mfabiashara, mama ntilie, machinga na tarehe 28 Oktoba ndiyo siku ya kuamua. Tukapige kura ya kutuondoa katika utawala huu,” amesema Lissu huku akishangiliwa

Lissu amesema “tukapige kura kwa ajili yenu weneywe, watoto wenu na wajukuu wenu, tutashinda hii habari na tutaishinda kwa kimbunga.”

Kuhusu majeshi, Lissu amesema “majeshi ya Tanzania, mnaona umati wa watu kila ninapokwenda, Watanzania hawataki kuona uchaguzi unaharibika, rai yangu kwenu, msije kugeuza silaha zenu dhidi ya sisi wananchi. Tukitengeneza nchi ya haki nanyi mpatapa haki zenu kama wengine.”

Akiwa Jimbo la Sumve kwenye uwanja wa Nyambiti, Lissu aliwaahidi wananchi endapo watamchangua atahakikisha anashughulikia gharama za chapa ya ng’ombe ambazo zimekuwa kero kwa wananchi, ushuru wa mazao unaowatesa wakulima, ujenzi wa barabara ya nyambiti pamoja na kuomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha inasimamia uchaguzi kwa weledi.

PLissu alihutubia mkutano wa Jimbo la Magu viwanja vya Kabila alizungumzia suala la uongozi usioridhisha wa watendaji wa kijiji na kuahidi kuushughulikia akiingia madarakani ili wananchi waweze kuipenda Serikali yao.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!