January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lishe ipewe kipaumbele-PANITA

Matunda ambayo ni sehemu ya Lishe Bora

Spread the love

SERIKALI ijayo imetakiwa kuliweka suala la lishe kuwa sehemu ya vipaumbele vyake. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na washiriki wa mkutano wa kujadili suala la lishe nchini.

Mkutano huo umeandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Partnership for Nutrition in Tanzania (PANITA) na kushirikisha wadau wa lishe wakiwemo wataalamu wa chakula na vyama vya siasa.

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Lydia Bendera, amesema “serikali inayoingia madarakani mwaka huu, lazima iweke lishe kuwa sehemu ya vipaumbele vyake. Pia ni lazima suala hili liwe endelevu sio kulizungumzia na kuliacha.”

“Tunaiomba wizara za Kilimo na Mifugo kuliangalia suala hili kwa undani na sio kila siku uwe wimbo. Tunapozungumzia suala la lishe, tuzungumzie kuboresha mlo mmoja kwa Watanzania kwa siku,” ameeleza Lydia.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA, Tumaini Mikindo amesema suala la lishe ni mtambuka, hivyo linahitaji wadau mbalilmbali kuungana na kuhakikisha hali ya lishe inaimalika nchini.

“Suala la lishe linahusu mambo ya fedha, elimu, ajira, wataalamu na rasilimali. Hivyo lazima makundi mbalimbali wakiwemo serikali, asasi zisizo za kiserikali, wadau wa maendeleo wakiwemo Umoja wa Mataifa (UN) kukaa pamoja na kuangali namna gani tunaweza kupunguza tatizo la njaa kwa pamoja,”ameeleza Mikindo.

error: Content is protected !!