August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lipumba, Msajili wasulubiwa

Spread the love

 

MAKUNDI ya kumpinga Prof. Ibrahim Lipumba na genge lake yameanza kujitokeza ambapo Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi (JUVICUF) imemuonya, anandika Pendo Omary.

Pia JUVICUF imemnyooshea kidole Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba ndiye anayechochea sintofahamu iliyopo ndani ya chama hicho.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Dahlia Majid, Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi – JUVICUF kwa niaba ya Hamidu Bobali mwenyekiti wa jumuiya hiyo inaeleza kuwa, maoni yaliyotolewa na Jaji Mutungi na yaliyompa nguvu Prof Lipumba kurejea uenyekiti wa chama hicho licha ya kujiuzulu Agosti mwaka jana ni ya kushinikizwa.

“Haiingii akilini kwa mwanasheria kama yeye (Jaji Mutungi) ambaye ana Katiba za vyama vyote apelekewe mzozo kisha aamue kisiasa badala ya kisheria tena kwa kurejea Katiba ya chama husika.

“JUVICUF tuna kila sababu ya kusema Msajili anatumika kutokana na kukiita Kikao cha Baraza Kuu na maamuzi yake eti ni batili tena bila kutoa vigezo,” amesema Majid.

Jumuiya hiyo imemtaka Jaji Mutungi kuwaomba radhi wanachama wa CUF kwa hatua aliyoichukua.

“Mwisho JUVICUF tunamtaka Prof. Lipumba na kundi lake la wahuni kuondoka mara moja katika ofisi za CUF, kwani kitendo walichokifanya cha kuvamia ni jinai kubwa.

“JUVICUF inatoa onyo na hadhari kwa maadui wa CUF wa ndani na nje ya chama kuwa, itapambana nao kwa hali yoyote kwani tupo kwa ajili ya kukilinda chama kupitia Katiba,” amesema Majid.

error: Content is protected !!