
Prof. Ibrahim Lipumba, Aliyekua Mwanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)
FREEMAN Mbowe, mwenyekiti mwenza wa umoja leo amemtuhumu Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), aliyerudishwa madarakani na Msajili wa Vyama Vya Siasa kwamba, amekuwa akifanya kafara kwenye Ofisi Kuu ya chama hicho, anaandika Charles William.
Mapema mchana wa leo katika tamko la viongozi wanaounda vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ilidaiwa kuwa Prof. Lipumba na wafuasi wake, wameigeuza Ofisi Kuu ya CUF Buguruni, jijini Dar es Salaam kuwa nyumba ya kulala wageni huku wakifanya vitendo vya kishirikina.
“Viongozi wa Ukawa hatuwezi kuruhusu ofisi ya CUF kuwa ‘guest house’. Yule bwana na wenzake wanalala, wanaamka na kupiga mswaki katika ofisi za chama huku wakifanya vitendo vya kiganga kwa kuchinja kondoo na kuvunja nazi,” amesema Freeman Mbowe wakati akisoma tamko la Ukawa.
Akiwa ameambatana wenyeviti wengine watatu wa vyama vinavyounda Ukawa pamoja na makatibu wakuu wa vyama hivyo Mbowe alitoa tamko lililosainiwa na wenyeviti wa vyama vyote vya Ukawa.
“Yule bwana amekula cha mtu na kazi aliyopewa hajaimaliza, anataka kurejea ili amalizie kazi yake kwa kushirikiana na Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama Vya Siasa,” amesema.
Hata hivyo, Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, aliyerudishwa madarakani na Msajili wa Vyama Vya Siasa haraka amejibu kwamba, tuhuma hizo hazina msingi wowote.
“Wameishiwa hoja hao, sisi tupo ofisini hapa, wanaofanya vitendo vya kishirikina ni kina nani? wanaotoa madai hayo wanapaswa kuthibitisha ukweli wa madai yao,” amesema Kambaya.
Si ajabu baabdi ya vijana wetu wakaogopa kusoma hadi kuwa maprofesa, kwa hofu kuwa wasije na wao wakaja kufanya madudu ya kufa mtu huku wakiwa wamejikausha kana kwamba wanafanya jambo la msingi.
Nimeona na kusoma maelezo ya baadhi ya viongozi wa kafu juu ya namnaa katiba ya CUF inavyoelekeza jinsi ya kujiuzuru, lakini sijaona wala kusikia namna mtu anavyoweza kurudi madarakani bila mkutano na vikao vilivyomweka madarakni awali kuhusika.
Je 1.upo utaratibu wa kujiuzuru kwa kuandika barua na kisha ukarudi madarakani kwa kuandika barua
tena kwa kadri utakavyojisikia?
2. Kama utaratibu huo upo, je, kuna mahali ambapo Masili wa vyama ametajwa kuwa anaweza
kuingilia kati na kuamua nani awe mwenyekiti wa chama fulani cha siasa.?
3. Kama utaratibu huo upo, ni nani anao; Msajili wa vyama, au katiba ya chama au sheria ya
vyama vya siasa?