January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Limbu amng’ang’ania ‘Zitto’

Katibu mkuu wa Chama cha ACT-Tanzania Samson Mwigamba

Spread the love

LUCAS Limbu, mwenyekiti wa Chama cha Alliance for change and Transparence (ACT), ameendelea kung’ang’aniza kuwa Samson Mwigamba na Prof. Kitila Mkumbo, siyo wanachama wa chama hicho. Sarafina Lidwino, anaandika.

Limbu, mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa na ambaye anatambulika na Sheria Na. 5 ya vyama vya siasa anasema, Prof. Kitila na Mwigamba, tayari wameshafukuzwa na hakuna mwenye ubavu wa kuwarejesha ACT-Tanzania.

Mwenyekiti alikuwa akizungumzia kinachoitwa “uchaguzi unaoendelea ndani ya chama” chake. Alisema ndani ya ACT kwa sasa, hakujawa na uchaguzi.

“Nikiwa mwenyekiti halali wa chama hiki, naomba ieleweke wazi kwamba, bado hatujatangaza taratibu za uchaguzi. Uchaguzi unaofanyika katika ngazi za vijiji na kata, siyo wa ACT- Tanzania. Huo ni uchaguzi wa chama cha Mwigamba na Prof. Kitila,” ameeleza.

Amesema, wanaotisha uchaguzi – Prof. Kitila na Mwigamba – siyo viongozi wala wanachama wa chama chake na hivyo hawana mamlaka ya kuitisha uchaguzi.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam.

Prof. Kitila na Mwigamba wamefukuza uanachama kwa makosa ya kuanzisha chama ndani ya chama.

Chama cha ACT kinachoongozwa kinyemela na Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini; Mwigamba na Prof. Kitila, ni mawakala wake.

Limbu amewataka wanachama wa ACT wawe watulivu, wakati ofisi ya msajili wa vyama ikiendelea kupitia nyaraka zao za mabadiliko ya uongozi.

error: Content is protected !!