May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lil Baby kumsaidia Jack Boy ujenzi wa hospitali Haiti

Spread the love

 

RAPA kutoka Marekani, Dominique Jones ‘Lil Baby’ amejitolea kumsaidia Msanii Pierre Delince (Jack Boy) katika ujenzi wa hospitali huko nchini Haiti. Anaripoti Glory Massamu, TUGARCo … (endelea).

Ambapo kupitia Insta stori ya Jack Boy aliposti ujumbe unaosema “Nimepita hospitalini huko Haiti wagonjwa wote wanalala nje… nimekabidhi fedha kusaidia ujenzi wa hosptali lakini nahisi kama haitoshi, nani anataka kuungana na mimi kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ukizingatia sio kitu kikubwa sana kwetu sisi tunaotumia dola?”

Lil baby alijibu ujumbe huo na kusema ataungana naye ambapo Jack Boy alimjibu kwa kusema;

“Kwa upendo huu umepata aina nyingine ya heshima kutoka kwangu…nitapanga kila kitu ili uweze kuwasiliana na Mkurugenzi wa Hospitali.”

Hata hivyo Jack Boy alishea maongezi hayo kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika; “Nimepata mwenzangu kwenye hili na Mungu akipenda tutajenga kitu cha pekee.”

error: Content is protected !!