October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lijualikali, Prof. J wapanda jukwaa la JPM

Spread the love

PETER Lijualikali, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero (Chadema) na Joseph Haule (Prof. J), Mbunge wa Mikumi (Chadema), wamemwagia sifa Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wakiwa kwenye uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa handaki sehemu itakayopita treni ya kisasa, Kilosa mkoani Morogoro unaofanywa na Rais Magufuli, Lijuakali ndiye aliyeanza kupewa nafasi ya kuzungumza.

Rais Magufuli amesema, amefurahi kumuona Lijuakali kwenye hadhara hiyo leo tarehe 29 Juni 202. Alimwita alimwita kuzungumza kwenye hadhara hiyo akifuatisha wito kwa kila mbunge aliyepo kwenye shughuli hiyo kuzungumza.

“Nimefurahi kumuona Lijuakali, sasa utakuwa Lijuabaridi. Njoo uongee,” wakati akisogea kwenye kipaza sauti, Rais Magufuli alimwambia “umeanza kupendeza vizuri.”

Akizungumza baada ya kupewa nafasi, Lijualikali alimsifu rais kwamba mambo anayofanya ni makubwa na kwamba, yeye (Rais Magufuli) ni barakwa kwa Watanzania.

“Mheshimiwa rais, unafanya kazi kubwa sana, Watanzania wote wanaona kazi unayoifanya. Hakuna dhambi yoyote unayoifanya, na kama ipo basi ni kujenga dude hili (reli-SGR), ni kupeleka umeme kila kijiji.

“Mimi naamini hii si dhambi, ni Baraka za Mungu ametupa, watu wanakulalamikia lakini ni kwa sababu wana mipango yao,” amesema Lijuakali.

Rais John Magufuli

Akitumia jukwaa hilo hilo, Prof. J alianza kwa kuwataka wakazi wa Kilosa waliohudhuria uwekaji jiwe la msingi huo kupasha na kisha kumpigia makofi matatu Rais Magufuli.

“Mheshimiwa rais, heshima kubwa kutoka kwa kijana wako al-maarufu Prof. J, mbunge anayeongoza binadamu na wanyama, ngwiii ngwiii! “Nimesimama kama mwakilishi wa wana Kilosa kwa ujumla, umma huu mheshimiwa rais unaonesha ni kwa jinsi gani ulikuwa na matumaini makubwa sana kukuona.

“Ndugu zangu wa Kilosa naomba tumkaribishe mheshimiwa rais kwa kupekecha mikona-pasha pasha pasha, piga makofi matatu pwa pwa pwa! Hayatoshi, piga makofi matatu

Akizungumza kazi alizofanya Rais Magufuli, Prof. J ameshukuru kwa ujenzi wa barabara ya kutoka Dumila mpaka Kilosa. Hata hivyo, ameomba kukamilishwa kwa kilomita 78 za barabara hiyo kutoka Kilosa kuelekea Mikumi.

Amsema, wana Kilosa wana changamoto kubwa ya mashamba na kwamba, wamekuwa wakizungumza na Willium Lukuvi, Waziri wa Ardhi ambye aliwambia mashamba hayo yako mezani kwake.

“Tunaomba mashamba haya (yanayomilikiwa na wageni) yafutwe na kisha tuwape wananchi hawa ili tuepuke migogoro ya wakulima na wafugaji,” amesema.

Akizungumzia Bwawa la Kidete, Prof. J amesema, bwawa hilo lilipasuka na kusababisha mafuriko ya mara kwa mara, amemuomba Rais Magufuli ajenge bwawa hilo.

“Tunakuomba mheshimiwa rais kwa unyenyekevu, tuko chini ya miguu yako, utujengee bwawa hilo la Kidete. Wana Kidete wanalia kwa sababu mafuriko yote ya Kilosa yanatokana na Bwawa la Kidete kwa kuwa limezidi kwa maji mengi.

“Kuna Mto Muyombo ambao umepoteza uelekeo kutokana na maji yamezidi, tunaomba mtujengee ili kuepusha mafuriko katika Wilaya ya Kilosa.”

Akizungumzia posho za madiwani wa CCM, Prof. J amemwomba Rais Magufuli kuhakikisha madiwani hao wanapata posho hizo kwa kuwa, walisaidia kwenye vikao vya maendeleo ya wilaya hiyo.

“Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa inaongozwa na Chama Cha Mapinduzi, madiwani wa Chama Cha Mapinduzi waliomaliza muda wao wamenituma, wanasema mpaka leo hawajapata bahshishi yao.

“Mheshimiwa rais, naomba uwakumbuke madiwani hao waliofanya kazi kubwa katika Wilaya ya Kilosa ili iweze kuendelea,” amesema.

Baada ya Prof. J kumaliza kuongeza, Rais Magufuli alimshuku huku akisema “asante sana, nimefurahi ulipopiga (kunja) ngumi hivi, nikaona hiyo ni dalili nzuri ya CCM oyee!”

error: Content is protected !!