Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lijualikali: Nimepata mateso makali Ukonga
Habari za SiasaTangulizi

Lijualikali: Nimepata mateso makali Ukonga

Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero
Spread the love

PETER Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, (Chadema) amesema akiwa mfugwa kwa yake kwa siku 79 katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, aliteswa na kunyimwa haki zake, anaandika Pendo Omary.

Lijualikali ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online leo mchana baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”

“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.

“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.

“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.

Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”

Ameeleza kuwa wakati akifanyiwa vitendo vya kikatili na baadhi askari wa jeshi hilo, asilimia kubwa ya wafugwa walimpokea vizuri na walimpa ushirikiano.

Amesema: “Wafugwa ni watu wazuri, wamekuwa ni walimu wangu, wazazi wangu, washauri wangu na wasiri wangu. Walinipa mashuka.

“Walinipikia chakula pale walipoona nashidwa kula chakula kilichopikwa kwa ajili ya wafugwa. Ambacho ni dagaa waliojaa mchanga na dona tena lililosagwa na mabuzi ya mahindi. Walinisaidia kazi nzito. Ingawa wapo baadhi ambao tulikuwa hautuelewani. Nadhani ni sababu za kisiasa,” ameeleza Lijualikali.

Lijualikali amesema Tanzania bado ina safari ndevu kufikia nchi ambayo inaamini katika uhuru, haki na demokrasia kwa maana halisi. Hivyo amewataka Watanzania kuacha kunyamazia ukiukwaji wa haki dhidi ya raia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!