Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lijualikali: Mbowe alikuwa kalewa, hakushambuliwa
Habari za Siasa

Lijualikali: Mbowe alikuwa kalewa, hakushambuliwa

Peter Lijualikali, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero
Spread the love

MBUNGE wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali amesema, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe hakushambuliwa na watu wasiojulikana bali alidondoka katika ngazi akiwa amelewa. Amewatuhumu Chadema, kucheza michezo ovu dhidi ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Lijualikali amesema hayo leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la kumpongeza Rais wa Tanzania, John Magufuli jinsi alivyoendesha mapambano ya janga la corona.

“Kwa sababu tunataka kusema ukweli na ukweli utatuweka huru kama taifa,” amesema Lijualikali wakati akianza kuchangia

Amesema, amemsikilia Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akisema walikuwa nyumbani kwa Mbowe hadi jana Jumatatu hadi saa 1 usiku, “lakini baadaye walitoka na kwenda kulewa.”

Lijualikali amesema, Taifa liko katika mapambano ya janga la corona na Chadema wamekuwa wakifanya vikao kwa njia za kidigitali, “lakini chama hiki hiki. Mchungaji Peter Msigwa amenukuliwa anasema walikuwa katika kikao na Mbowe, lakini baadaye walitoka na kwenda kulewa” kwa hiyo watu wanapaswa kusema ukweli.

Huku akishangiliwa na wabunge wa chama tawala, LIjualikali amesema, “hili tukio la leo, Mbowe kapanda ngazi kaanguka, katereza kavunjika. Huu ni ukweli kabisa.”

Lijualikali amesema, kutokana na kitendo cha Mbowe kujua amelewa.. “hii michezo inafanyika na ukitaka kujua ni usanii, kwa nini amekwenda hospitali binafsi, hajakwenda ya umma, amejua akienda hospitali ya umma wangesema huyu alikuwa amelewa, kwa hiyo haya mambo tunayafanyaga.”

Akiendelea kuzungumza, Lijualikali amesema, “huyu mzee haumwi, huyu mzee hajapigwa, hajakanyangwa kanyangwa, kaanguka na kuvunja kifundo mcha mguu.”

Mbowe ambaye alikuwa amelazwa hospitali binafsi jijini Dodoma baada ya kudaiwa kushambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kumakia leo Jumanne akiwa katika makazi yake Area D jijini humo, amehamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Baada ya Lijualikali kumaliza kuchangia, Spika wa Bunge, Job Ndugai akasema, “haya mambo yanatuhusu sisi kwa sisi. Mtu aliyepigwa na kujeruhiwa hawezi kupelekwa kituo cha afya.”

Amesema, ameona barua mezani kwake kutoka kwa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ya kuomba ndege ya kumpeleka Mbowe Dodoma lakini kiongozi huyo wa Bunge akasema utaratibu ni lazima apewe rufaa na hospitali ya Serikali.

Spika Ndugai amesema, hilo halikufanyika na ,”tutaendeleza kutoa ushirikaino mwingine” pale utakapohitajika.

“Tusiingize siasa katika eneo ambalo siasa hakuna kabisa kabisa na ni vizuri polisi wakatoa taarifa haraka ya kile wanachokijua,” amesema Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!