August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi ya Congo kusitishwa sababu za kiusalama

Spread the love

KUFUATIA hali ya usalama kuwa tete nchini ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) hatimaye serikali kupitia Waziri wa michezo nchini humo, Denis Kambayi imelitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za Ligi Kuu iliyotakiwa kuchezwa siku ya Alhamisi kwa muda usiojulikana.

Kambayi amesema, serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ongezeko la vurugu katika viwanja vya soka na ukosefu wa uaminifu katika ukusanyaji wa mapato wakati kuna mechi uwanjani katika siku za hivi karibuni lakini pia kwa sababu za kisiasa.

Wasiwasi uliopo ni kuwa hali iliopo kwa sasa mtaani huwenda ikafika hadi uwanjani, dalili hiyo ilionekana siku chache za nyuma katika moja ya mechi iliyochezwa na huku mashabiki walikuwa wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika hali iliyowashangaza wengi.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuwa na tahadhali kwamba huwenda kukatokea vurugu katika viwanja vya mpira, pale muhula wa Rais wa sasa nchini humo Joseph Kabila utakapo fikia kikomo wiki ijayo huku kukiwa na dalili kwa kiongozi huyo kutotoka madarakani.

Kabila alitakiwa kung’atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi uliopita.

error: Content is protected !!