October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu Zanzibar kurejea Juni 5

Uwanja wa Mao Tse Tung

Spread the love

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu humo kuanzia Juni 5, 2020 baada ya kufanikiwa kukabiliana kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Akitangaza uamuzi huo leo tarehe 27 Mei, 2020, Makamu wa Pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na kuwaagiza Wizara inayosimamamia michezo sambamba na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Wizara ya Afya kuandaa utaratibu ambao utaisaidia kuendesha Ligi hiyo kwa tahadhali kubwa.

Ligi hiyo ambayo inashirikisha jumla ya timu 16 ilisimama Machi, 2020 kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa la kusimamisha shughuli zote za michezo nchi nzima kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuongezewa tena muda kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.

Katika hatua nyingine Serikali ya visiwani humo imesema kuwa michezo mingine yote inayochezwa na klabu, makundi na hata mmoja mmoja ikiwemo mashindano ya ufukweni hayataruhusiwa kwa sasa mpaka watakapotoa taarifa nyingine.

Mpaka ligi hiyo inasimama tayari ilishachezwa michezo 20 kwa baadhi ya klabu huku KMKM ikiwa kileleni kwenye msimamo ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza michezo 19, huku Chipukizi ikishika mkia kwa kuwa na pointi tisa, baada ya kucheza michezo 19.

error: Content is protected !!