May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu Bara kusimama wiki mbili

Spread the love

 

 Mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa tarehe 3 Juni, 2021 kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba, Ligi Kuu Tanzania Bara itakwenda mapumziko kwa wiki mbili kupisha kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania itakayotangazwa kesho na kocha mkuu wa kikosi hiko Kim Poulsen. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko kitakachotangazwa kesho kitaingia kambini mapema juni wa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu kombe la Dunia utakaopigwa Septemba 2021 mara baada ya ratiba kutoka shirikisho la mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA).

Katika kipindi hiko cha wiki mbili Taifa Stars itacheza michezo miwili ya kirafiki katika kujiweka sawa na mchezo huo wa kufuzu kwa michuano hiyo ya kombe la Dunia itakayofanyika Qatar kuanzia 12 Novemba hadi Disemba 18, 2022.

Katika ratiba iliyotolewa na bodi ya Ligi ya hivi karibuni imeonesha Ligi itapumzika mara baada ya mchezo kati ya Ruvu Shooting na Simba na kurejea tena tarehe 15 Juni, 2021 ambapo utapigwa mchezo mmoja kati ya Biashara United dhidi ya Namungo FC.

Kwa upande wa Yanga wao watalazimika kusubiri hadi tarehe 17 Juni, 2021 ambapo watashuka tena dimbani kuwakabili Ruvu Shooting mara baada ya kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu tarehe 19 Mei 2021 dhidi ya Jkt Tanzania amber waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

error: Content is protected !!