December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu bara kurejea leo, viwanja viwili kuwaka moto

Spread the love

 

NBC PremierLeague inarejea leo Jumamosi tarehe 16 Oktoba, 2021 kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Saa 8:00 mchana katika uwanja wa Kaitaba – Bukoba, Kagera Sugar FC wakiwa na alama moja baada ya kucheza michezo miwili, watapepetana na Mbeya City FC wenye alama 4.

Aidha, saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Nyankumbu wilayani Geita mkoani Geita, matajiri wa dhahabu Geita Gold FC wakiwa wamepoteza michezo yote miwili ya awali, wataumana na wakata miwa wa Mtibwa Sugar wenye alama moja.

Katika msimu mpya wa Ligi ulioanza kutimua vumbi Septemba 27 mwaka huu, timu za Yanga na Polisi Tanzania ndio wanaoongoza ligi hiyo kwa kufungana alama sita huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara mbili.

Je, leo ni timu gani kuondoka na alama 3?

error: Content is protected !!