Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Ligi Kuu Bara kurejea Juni 13, 2020
Michezo

Ligi Kuu Bara kurejea Juni 13, 2020

Spread the love

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametangaza tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ni Juni 13, huku ratiba kamili ikitarajiwa kupangwa Mei 31, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kuendelea kwa michezo hiyo ni kufuatia agizo la Rais John Magufuli kutanga shughuli za michezo kuendelea kufuatia kuwepo kwa mwenendo mzuri wa mlipuko wa ugonjwa Corona nchini.

Taarifa ya kuendelea na michezo hiyo kutoka bodi ya Ligi imetolewa kwenye kurasa yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuwa na vikao vya muda mrefu na kusubiri muongozo kutoka Serikalini.

Baada ya agizo hilo baadhi ya klabu mbalimbali wa Ligi Kuu tayari zimeanza maandalizi ya kumalizia michezo iliyosalia ambayo itachezwa katika kituo kimoja Jijini Dae es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex.

Ligi hiyo ilisimama mwezi Machi kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kutaka shughuli zote za michezo kusimama kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, huku klabu ya Simba ikiwa vinara kwenye msimamo wakiwa na alama 72.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!