Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo Ligi Kuu Bara kurejea Aprili 8
Michezo

Ligi Kuu Bara kurejea Aprili 8

Mbeya City
Spread the love

 

BAADA ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimama kupisha michezo ya kimataifa na maombolezo, sasa itaendelea tena Aprili 8, 2021 kwa michezo miwili itakayochezwa kwenye viwanja tofauti. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo wa wa mwisho wa ligi hiyo ulichezwa Machi 10, 2021, uliowakutanisha Simba dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkapa na kusimama kwa wiki mbili kupisha michezo ya kimataifa kufuzu AFCON kati ya Taifa Stars dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Tarehe 18 Machi 2021, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilisitisha michezo yote kwa siku 21 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.

Magufuli alifariki tarehe 17 Machi, 2021 majira ya saa 12 jioni kwenye hospitali ya Mzena iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam na kifo chake kilitangazwa na aliyekuwa Makaumu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ratiba iliyotolewa hii leo na bodi ya Ligi imeonesha kuwa mzunguko wa 25 utaendelea kuanzia Aprili 8, kuanza na mchezo namba 221.

Katika siku hiyo michezo miwili itapigwa ambapo Mbeya City itakuwa nyumbani kuikabili Kagera Sugar na Namungo FC watamenyana na Ihefu kwenye Uwanja wa Majaliwa.

Ligi hiyo pia itaendelea Aprili 9, kwa kupigwa michezo mitatu ambapo itazikutanisha timu ya Biashara United dhidi ya Mtibwa, JKT Tanzania wataikaribisha Mwadui huku Azam FC wakiwa Chamazi Complex wataialika Mtibwa Sugar.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo klabu ya Yanga watashuka dimbani tarehe 10 Aprili, 2021 kumenyana na KMC kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa majira ya saa 1 usiku.

Mpaka Ligi hiyo inasimama Yanga walikuwa kileleni kwa pointi 50, huku wakifuatiwa na Simba kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 46, kwa tofauti ya michezo mitatu na vinara hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!