May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu Bara kurejea 13 Februari

Spread the love

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kurejea tena tarehe 13 Februari, 2021 mara baada ya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani ambayo Tanzania (CHAN) nayo ni washiriki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Taarifa kutoka ndani ya bodi ya Ligi imeeleza kuwa Ligi hiyo itaendelea kwa mzunguko wa 19 kuanzia tarehe hiyo huku ikiwakumbusha klabu zote zinashiriki kuanza maandalizi.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa michezo yote ambayo iliahirishwa (viporo) kutokana na baadhi ya timu kushiriki kwenye michuano ya CAF itachezwa kuanzia tarehe 4 Februari 2021 na baadae kuendelea na mzunguko wa kawaida.

Msimamo wa Ligi hiyo mpaka inasimama inaonyesha timu ya Yanga kuwa kileleni kwa pointi 44 baada ya kucheza michezo 18, huku ikifuatiwa na Simba yenye pointi 35 ikiwa na michezo 15, na nafasi ya tatu ikishikwa na Azam FC yenye pointi 32 baada ya kucheza michezo 17.

error: Content is protected !!