August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu bara kuendelea kesho

Wachezaji wa viongozi wa African Lyon wakishangilia moja ya ushindi waliopata katika michezo yao

Spread the love

BAADA ya mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi, hatimaye Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena kesho na kesho kutwa, kwa kupigwa michezo minne katika viwanja vitatu tofauti, ikiwa ni raundi ya tatu toka kuanza kwa mzunguko wa pili.

Mabingwa watetezi Yanga ambao wana kumbukumbu ya kutoa sare kwenye mchezo uliopita wa ligi hiyo dhidi ya Africa Lyon, watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara, mchezo unaotarajia kufanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Siku hiyo hiyo, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manungu, Desemba 29, kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru, huku Azam FC ambayo haina matokeo mazuri kwa hivi sasa itacheza na Tanzania Prisons ya Mbeya katika dimba la Chamazi.

Michezo hii itakuwa ya mwisho kwa klabu za Simba, Yanga na Azam kabla ya kuelekea kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza siku ya Ijumaa kwa kuanza na mchezo wa ufunguzi kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys.

error: Content is protected !!