Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Biashara Licha ya uwepo wa corona, Benki Exim yatangaza faida
Biashara

Licha ya uwepo wa corona, Benki Exim yatangaza faida

Spread the love

 

BENKI ya Exim (Group) imetangaza kupata faida ya jumla ya Sh.25.3 bilioni (kabla ya kodi) kwa mwaka 2020, ikilinganishwa na hasara ya Sh.8.4 bilioni iliyopata kwa mwaka uliopita. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mafanikio hayo yanayotajwa kuwa yametokana na ufanisi wa kiutendaji licha ya changamoto za kiuchumi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, ulioathiri ukuaji wa uchumi kwa baadhi ya sekta muhimu mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo Alhamisi tarehe 4 Februari 2021, imebainisha benki hiyo imetekeleza kwa ufanisi mkakati wa kushirikiana na sekta zinazofanya vizuri sambamba na kuongeza umakini katika matumizi yake ili kuongeza tija zaidi katika utendaji.

“Katika kipindi hicho, benki ilikuwa bega kwa bega na sekta zilizoathiriwa wakati wa janga hilo, kwa kweli tulishirikiana kikamilifu na wateja wetu kuhakikisha kwamba si tu tunawapatia fedha bali pia tunawajengea uwezo wa kuweza kufanya shughuli zao katika kipindi hicho kigumu,’’ amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa wa benki hiyo, Jaffari Matundu.

Matundu amesema, hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2020, benki hiyo ilikuwa imetoa msamaha wa zaidi ya S.290 bilioni kwa njia ya likizo ya malipo na upanuzi wa vipindi vya ulipaji wa mikopo ili kusaidia wateja wa benki hiyo ambao biashara zao ziliathirika zaidi na athari za kiuchumi za Covid-19.

“Tunayo furaha kuripoti matokeo mazuri kwa mwaka wa fedha 2020. Tumefanikiwa kurejesha asilimia 9.0 ya faida kwenye mfuko wa wanahisa ikilinganishwa na marejesho hasi ya asilimia 9.2 mnamo 2019” amesema Matundu katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Nchini Tanzania, benki hiyo ilirekodi mafanikio makubwa kwa kupata faida (kabla ya kodi) ya Sh.18.8 bilioni kutoka kwenye hasara ya Sh.14.5 bilioni (kabla ya kodi) ya mwaka uliopita.

“Mafanikio hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa mali kufuatia usafishaji uliofanywa katika kipindi hicho cha mwaka uliopita hatua iliyosababisha kupungua kwa mikopo chechefu kutoka asilimia 22.3 ya mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 7.4 kwaka 2020.”

“Matawi yetu ya nchini Djibouti na Comoro pia yalirekodi faida ya Sh.4.9 bilioni na Sh.5.7 bilioni (kabla ya kodi) licha ya athari ya COVID-19.

“Jumla ya mali zetu imebaki Sh.1.9 trilioni. Amana za wateja zimeongezeka kwa asilimia 4.4 wakati wa robo ya mwaka na kufikia Sh.1.38 trilioni. Shughuli zetu nchini Tanzania, Comoro na Uganda zote zimerekodi ukuaji wa ajabu katika amana za wateja wakati wa robo ya mwisho wa mwaka,” amesema

Amesema, mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na kauli mbiu ya benki hiyo “Exim Kazini Leo kwa ajili ya Kesho’ ambayo imekuwa ikiisukuma benki hiyo kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja wake

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini...

BiasharaHabari

NMB yavutia wabunifu suluhisho za kifedha, Dk. Mpango agusia vijana

Spread the love  MFUMO wa majaribio wa suluhishi za kifedha ulioandaliwa na...

BiasharaHabari

NMB Nuru Yangu yazinduliwa, 200 kunufaika

Spread the loveBENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi...

BiasharaHabari

Waziri Bashe uso kwa uso vigogo NMB bungeni

Spread the loveWAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amekutana na kufanya...

error: Content is protected !!