October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Licha ya kupingwa na Ethiopia, Tedros mgombea pekee WHO

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO

Spread the love

 

MKUU wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus anaweza kuwa mgombea pekee katika nafasi anayoshikilia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Vyanzo vya taarifa vinasema, ni namna gani atateuliwa kabla ya muda wa mwisho wa uteuzi wiki ijayo, ni jambo ambalo haliko bayana katikati mwa upinzani kutoka serikali mjini Addis Ababa.

Tedros anawania muhula wake wa pili, wakati huu ambapo anajaribu kuiongoza dunia, kupita katika mzozo mkubwa zaidi wa kiafya katika karne.

Tedros ambaye ni waziri wa zamani wa afya wa Ethiopia anayetokea mkoa wa Tigraya, alichaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa WHO Afrika mwaka 2017. Amekuwa mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo.

Muethiopia huyo analiongoza shirika hilo kupita milipuko kadhaa ya ugonjwa wa Ebola na pia janga la Covid – 19 akinusurika ukosoaji mbaya kutoka utawala wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa madai ya “kuipendelea China.”

Wakati hajakiri hadharani kuhusu mipango yake ya kuwania tena muhula wa miaka mitano, akisema amejielekeza kwenye kupambana na janga la Covid-19, vyanzo vinne vilisema, ndiye mgombea pekee anaejulikana mpaka sasa.

Mtoa taarifa ambaye amekataa kutajwa jina lake kutokana na usiri wa mchakato huo, na ambaye anaufahamu wa moja kwa moja wa mchakato wa uchaguzi amesema, “Tedros kwa uhakika ni mgombea,” na kuongeza, “kwa hatua hii, hakutakuwa na mgombea mbadala.”

Hata hivyo, Tedros, ambaye Jenerali mmoja wa Ethiopia amuita hadharani kuwa “mhalifu” na kumtuhumu kwa kujaribu kununua silaha kwa ajili ya vikosi vya Tigray, hatarajiwi kuteuliwa na nchi yake kama ulivyo utamaduni wa kidiplomasia, maafisa wawili wa Ethiopia waliliambia shirika la Reuters.

Billene Seyoum, msemaji wa waziri mkuu, na Dina Mufti, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia, hawakupatikana kujibu madai hayo.

error: Content is protected !!