LICHA ya kupoteza kwa mabao 3-1, kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Costo De Agosto kutoka Angola, timu cha Namungo FC imefuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Namungo FC imefanikiwa kufuzu kwenye hatua hiyo ya makundi kwa jumla ya mabao 7-5, mara baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa mabao 6-2, uliofanyika kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Katika mchezo huo wa leo uliofanyika pia kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi, Costo De Agosto walikuwa wanajaribu kujiuliza kuona kama watafanikiwa kupata idadi kubwa ya mabao ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata lakini mambo yalionekana kuwa magumu.
Kwa matokeo hayo Namungo itaangukia kundi D, sambamba na Raja Casablanca kutoka Morocco, Pyramids ya Misri pamoja na Nkana Red Devil kutoka Zambia.
Leave a comment