August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LHRC yataja mwarobaini changamoto mchakato wa katiba kuvurugwa na wanasiasa

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetoa mapendekezo manne juu ya namna bora ya ufufuaji mchakato wa upatikanaji katiba mpya uliokwama 2015, huku kikisitiza wananchi kuwa mstari wa mbele ili kudhibiti wanasiasa kuukwamisha kwa kuweka maslahi yao mbele. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mapendekezo hayo yalitolewa jana Ijumaa na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, akizungumza na wanahabari, jijini Dar es Salaam, kuhusu maamuzi ya Halmashauri Kuu ya chama tawala cha CCM, kubariki ufufuaji wa mchakato huo.

“Suala la katiba sio la vyama, lakini kwa mujibu wa katiba yetu tuliyonayo ambayo tunataka ibadilike, ili ushiriki mchakato wa maamuzi lazima upitie kwenye vyama. Vyama vimekubali sasa inawezekana. Lazima itungwe sheria ambayo itafufua mchakato kwa kuunda Bunge Maalum la Katiba,” alisema Henga.

Henga alisema “endapo bunge litaundwa, uwekwe uwakilishi mpana wa wananchi zaidi ya wabunge, ili kurudisha imani ya wananchi juu ya mchakato wa katiba mpya na kuwapa uhakika kuwa, masuala yao yanazingatiwa vyema kuliko kuzingatia maslahi zaidi ya wanasiasa.”

Mbali na wito huo, Henga alitoa mapendekezo manne juu ya ufufuaji wa mchakato huo, la kwanza likiwa ni Serikali kupeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 8 ya 2011, ili iendane na wakati.

Pendekezo la pili, Serikali ipeleke muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11 ya 2013, ili nayo pia iendenane na wakati, huku la tatu likiwa Bunge Maalum la Katiba litakaloundwa, litumie Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba.

Wakati la mwisho likiwa Serikali kufungua milango ya majadiliano, ili wananchi watoe maoni yao kuhusu marekebisho ya katiba.
“Bunge Maalum litakaloundwa litumie rasimu ya pili ya katiba, maarufu kama Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Sababu mpaka rasimu ya pili inaundwa hakukuwa na ugomvi, ugomvi ulikuja kwenye katiba pendekezwa. Ingawa sio mbaya kama watachukua rejea za katiba pendekezwa,” alisema Henga.

Henga alitaja sababu zilizopelekea mchakato huo ulioanzishwa 2010 na Serikali ya Awamu ya Nne ,chini ya Rais Jakaya Kikwete na kukwama katika hatua ya kura ya maoni 2015 kwa ajili ya wananchi kuipitisha, ikiwemo kuingiliwa na maslahi ya kisiasa.

Henga alisema maslahi ya kisiasa yalivuruga mchakato huo, ilipoibuka hoja ya muundo wa Serikali, ambapo wanasiasa walijigawa kwa kundi moja kutaka Serikali mbili huku lingine likitaka Serikali tatu.

LHRC yataja muarobaini changamoto mchakato wa katiba kuvurugwa na wanasiasa.

error: Content is protected !!