Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Maisha Afya LHRC yapinga kufutwa Toto Afya: Ni ukiukaji wa sheria za watoto
Afya

LHRC yapinga kufutwa Toto Afya: Ni ukiukaji wa sheria za watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa vikali hatua ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kuondoa usajili wa bima ya Toto Afya na kueleza kuwa ni ukiukwaji wa sheria za watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

LHRC imelaani hatua hiyo ikiwa ni siku moja tangu mfuko huo kutangaza mabadiliko ya utaratibu wa kusajili watoto kupitia Toto Afya Kadi na badala yake watalazimika kuingizwa kama wategemezi kwenye bima za wazazi wao au kupitia taasisi za elimu.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumanne tarehe 14 Machi 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, kitaaluma ni wakili, alisema uamuzi huo ni kinyume na kifungu cha 8 cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Pia ameongeza ni kinyume na Ibara ya 24 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989 na Ibara ya 14 ya Makataba wa Adrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa mwaka 1989.

Henga alisema utaratibu wa bima ya afya ya Toto Afya Kadi umekuwa msaada wa mamilioni ya watoto wa kitanzania wasio na uwezo wa kumudu gharam,a za matibabu na ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakisaidiwa na wasamaria wema. Hata hivyo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga, kuna jumla ya watoto 200,000 waliounganishwa na Toto Afya tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015.

“Hatua hii ya Serikali kusitisha mfumo wa bima wa Toto Afya Kadi utaathiri watoto wengi hii ni kutokana na ukweli kwamba ni asilimia chache mno ya wazazi ambao wapo kwenye mfumo wa ajira rasmi,” amesema.

Ameongeza kuwa ni wazazi wachache wanaoweza kumudu gharama za vifurushi ambavyo NHIF imependekeza wazazi kujiunga.

“Tunatoa wito kwa Serikali kutazama upya madhara ya uamuzi wake ili kuhakikisha kwamba haki ya afya kwa watoto wa kitanzania inalindwa,” alisema Henga.

Kwa mujibu wa tovuti ya NHIF kifurushi cha chini za wazazi wenye watoto wanne ni Sh 816,000 huku cha juu kikiwa Sh 2,220,000 kwa kuzingatia umri wa wazazi.

Gharama ya Toto Afya Kadi ilikuwa ni Sh 50,400 kwa mwaka kwa mtoto mmoja ambaye mzazi aliweza kumsajili moja kwa moja NHIF bila yeye kulazimika kijiunga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

Afya

Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane

Spread the love  JUMLA ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya...

Afya

Naibu Waziri awabebesha Wakurugenzi zigo la miradi chini ya kiwango

Spread the loveIMEELEZWA kuwa usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo na ujenzi...

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

error: Content is protected !!