June 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

LHRC yaonya picha za utupu, kutisha

Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba (kulia) akiteta jambo na na Jaji Joseph Warioba

Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kuchapisha picha za utupu ama za kutisha katika mitandao ya kijamaa, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam na Dk. Helen Kijo Bisimba, Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu amesema kuwa, kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya kurekodi na kupiga picha ambazo sio nzuri kwa mujibu wa sheria.

Amebainisha picha hizo kuwa ni pamoja na matukio ya mauaji, ajali za kutisha na miili ya marehemu zinazochapichwa katika mutandao ya kijamii, blog na hata baadhi ya vyombo vya habari bila kijali kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Dk. Kijo amesema kuwa, tarehe 4 Mei mwaka huu katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo picha za miili ya marehemu (mama na mtoto) ambayo majina yao yamehifaziwa, zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha majeraha ya kutisha   kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa.

Katika tukio la pili amebainisha kuwa, ilitokea Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu ambapo picha za maiti ya mtoto aliyeuawa na mama wa kambo zilionesha akiwa ndani ya jeneza.

Katika maeneo ya Kibamba Jiji Dar es Salaam, Januari mwaka huu picha za utupu za mwanamke aliyesemekana kuwa ni msukule aliyekutwa kwenya kisima zilizambaza katika mitandao ya kijamii.

Amesema kuwa, hayo ni baadhi ya matukio hivyo jamii inapaswa kutambua kuwa vitendo hivyo ni udhalilishaji na kinyume cha sheria.

“Kwani kwa mujibu wa haki ya kikatiba ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kila mtu ana haki ya kikatiba ya kuthamini utu wake kuwa faragha akiwa hai au amefariki,” amesema.

error: Content is protected !!