January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LHRC yaonesha njia Viti Maalum

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Ofisa Mipango wa Jinsia na Watoto wa LHRC, Naemy Sillary

Spread the love

WABUNGE wa Viti Maalum wametakiwa kuhakikisha kuwa, utaratibu wa kuwapata unawekwa kisheria ili wasidharauliwe na jamii. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mkurugenzi wa Utetezi wa Kituo cha Haki za Binadamu nchini (LHRC), Harold Sungusia, amesema hayo jana alipokuwa akijibu hoja za wabunge mbalimbali katika semina ya uelewa wa mchakato wa uchaguziiliyofanika Dodoma.

Semina hiyo ipo chini ya Bunge kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UDNP).

Sungusia amesema, ili kuondoa dharau kwa viti maalum mambo ya msingi ya kuyafanya ni kuweka utaratibu muafaka utakaowekwa katika sheria wa jinsi ya kuwapata wabunge.

“Pia majukumu ya wabunge yajulikane kisheria ili waweze kuwajibika katika eneo hilo walililopangiwa,”amesema.

Aidha, ametaka elimu itolewe kwa umma ili waewelewe upatikanaji wa wabunge hao na majukumu yao ni yapi.

Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Zahara Ali Hamad amesema, Katiba imetoa

Viti Maalum kwa mkono mmoja lakini imekataa kwa upande mwingine.

Alitoa mfano kwa sheria inayotaka Waziri Mkuu atokane na Jimbo la Uchaguzi wakati mawaziri wengine wanaweza kutokana na jimbo ama Viti Maalum.

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara amesema, tabu kubwa ni wanawake wenyewe kutopendana.

“Tujitahidi kwanza kupendana wenyewe… Tutaona ni wanawake wangapi watampigia Asha-Rose Migiro kama si Lowassa (Edward Lowassa),” amesema Bungara.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Taulida Cassian Nyimbo amesema, kutopendana ni hulka ya mtu binafsi na wala sio wanawake.

“Siamini kuwa wanawake hatupendani, ukiweka mtu hauziki hawezi kupata hata kura za wanawake wenzake,” amesema.

Aidha amesema, Viti Maalum vimekuwa vikisumbua kwasababu watuhawafahamu jinsi gani vinapatikana.

Mwenyekiti wa semina hiyo, Anna Abdallah alitaka vyama vikubwa vya siasa kuonesha mfano kwa kuwapa wanawake vyeo katika vyama.

Hata hivo Mbunge wa Manyovu (CCM), Albert Ntabaliba amesema, ni vyema wanawake wakaanzisha vyama vyao vya siasa ili nafasi ya juu ziwe zao.

“Sijaona wanawake walioanzisha vyama vya siasa na sheria inaruhusu kufanya hivyo. Waanzishe ili wachukue nafasi zote za juu,” amesema.

error: Content is protected !!