July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LHRC yalaani mauaji Ngorongoro, yataka zoezi la mipaka kusitishwa

Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu kuishi na kutoa wito kwa serikali kusitisha zoezi la mipaka inayowekwa katika tarafa yua Loliondo wilayani Ngorongoro moani Arusha kwani sio shirikishi, limekosa uwazi na linavuruga amani na usalama. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Pia imeitaka Serikali kutoa taarifa juu ya watu wanaoshikiliwa na jeshi la polisi pamoja na taarifa za watu ambao hawajulikani walipo.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Fulgence Massawe jana tarehe 11 Juni, 2022 pia imetoa wito kwa Serikali kuchukua hatua za kisheria kwa watu waliohusika na mauaji ya askari aliyeuawa kwa kupigwa mshale juzi katika vurugu zilizoibuka katika tarafa hiyo.

Aidha, amesema kama kuna haja ya zoezi la kuweka mipaka kufanyika basi zoezi hilo liendeshwe kwa uwazi na kuzingatia sheria bila kusababisha madhara ya uvunjifu wa haki za biandamu.

“Kumekuwa na sintofahamu kuhusu zoezi la kuweka mipaka na kuwahamisha wananchi wa jamii ya kimasai katika eneo la Loliondo ili kuhifadhi eneo la kilometa za mraba 1,500 kwa ajili ya kulinda mazalia ya wanyama pori yanayotegemewa na mbuga ya Ngorongoro na Serengeti.

“Kwa namna ya kipekee LHRC imeona kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na zoezi zima limekosa ushirikishwaji wa jamii husika kitu kinachopelekea misuguano na vyombo vya dola katika kutekeleza zoezi hilo la kuweka mipaka,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwepo na taarifa za kujichanganya kuhusu zoezi linaloendelea eneo hilo kutoka kwa wananchi na serikali yenyewe.

Amesema wakati taarifa za wananchi na mitandao ya jamii inaonesha hali si shwari na kuna watu wamejeruhiwa serikali imeendelea kusisitiza hali ni shwari.

“Mbali na kudai hali ni shwari Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amethibitisha tukio la mauaji ya askari wa Jeshi la polisi aliyepigwa mshale katikia eneo la mgogoro. Kauli hii inakinzana na msimamop wa serikali kuwa hali ni shwari.

“Ni wazi kuwa tukio hilo na matukio mengine ya uvunjifu wa haki za kuishi kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania ya mwaka 1997,” amesema

Aidha, amesema kumekuwapo na taarifa zilizoripotiwa na wananchi kuhusu watu waliokamatwa na jeshi la polisi katika kata saba na hawajulikani wapo katika kituo gani mpaka sasa.

Watu hao wanatoka katika kata za Malambo, Piyaya, Arash, Oloirien, Oloypiri, Soit sambu, Ololosokwan.

Pia amesema kuna taarifa ya mwenyekiti wa kijiji cha Oloirien, madiwani wawili wa viti maalum na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngorongoro hawajulikani walipo hadi sasa.

error: Content is protected !!